IQNA

Msomi aangazia suluhisho za Mapinduzi ya Kiislamu kwa migogoro ya kisasa 

18:22 - September 05, 2025
Habari ID: 3481185
IQNA – Mwanazuoni mwandamizi kutoka Iran amesema kuwa kulinganisha mtazamo wa Tauhidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mtazamo wa kisekula wa Magharibi kunasaidia kufichua kwa undani vipengele vya migogoro ya dunia ya leo.

Katika makala kwa ajili ya IQNA, Ayatullah Abbas Kaabi, Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Wahadhiri wa Vyuo vya Kiislamu (Hawzah) nchini Irana mjumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu, alichambua mizizi ya migogoro ya ustaarabu wa Magharibi na suluhisho la Mapinduzi ya Kiislamu katika kukabiliana na hali hiyo.

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu 

“Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.”(An-Nahl: 36)

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa “tetemeko la ustaarabu” lililobatilisha dhana ya “kifo cha Mungu” na kuondolewa kwa dini katika uwanja wa kijamii na kisiasa. Leo hii, kulinganisha mtazamo wa Tauhidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mtazamo wa kisekula wa Magharibi kunadhihirisha kwa uwazi zaidi migogoro ya ulimwengu wa kisasa. Tauhidi ni kumpwekesha Menyezi Mungu katika Ibaada, Kumuabudu yeye peke yake, bila ya Kumshirikisha na kitu Chochote.

Magharibi: Ustaarabu Ulioondoa Mungu Katika Usimamizi wa Maisha

Ustaarabu wa kisasa wa Magharibi, kwa msingi wa kisekula, uliiondoa dini katika maisha ya umma na kuanzisha masanamu mapya kwa binadamu:

Sanamu ya ubepari: Utawala wa makampuni makubwa ya kifedha, makundi ya kifisadi na himaya za unyonyaji umeiteka siasa na uchumi wa dunia. Nyuma ya maamuzi ya kisiasa, utawala wa pesa, nguvu na unafiki hutawala. Matabaka, ubaguzi na ukosefu wa usawa wa kimfumo ni matokeo ya moja kwa moja ya sanamu hii.

Sanamu ya starehe: Kipaumbele cha ubinafsi na kutafuta raha kupita kiasi kumezalisha utumwa mpya kwa mwanadamu wa kisasa. Maana halisi ya maisha na raha ya kweli – hasa ndani ya familia – vimeporomoka.

Sanamu ya ubabe: Mafirauni wa zama hizi wamejenga mifumo ya kiusalama ya kifirauni na utawala wa dunia wa upande mmoja kwa kauli ya “Mimi ndiye Mola wenu Mkuu.” Kudhalilishwa kwa mataifa huru, uchochezi wa vita, mauaji ya halaiki na umwagaji damu katika uhusiano wa kimataifa vimekuwa viwango vya siasa na utawala.

Matokeo ya njia hii ni kuzalishwa kwa migogoro tata: migogoro ya utawala dhalimu, migogoro ya kiroho, migogoro ya usalama, kuporomoka kwa familia, msongo wa mawazo, ukosefu wa usawa wa kijamii, migogoro ya mazingira, na hatimaye, kifo cha ubinadamu – mfano dhahiri ukiwa ni jinai zinazofanyika Gaza. Magharibi ya kisekula imepoteza dira ya kweli na kuiacha dunia katika hali ya kughafilika na mkanganyiko.

Mapinduzi ya Kiislamu: Kurejea kwa Mungu na Dhana ya Hayat Tayyiba

Kwa upande mwingine, Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kauli mbiu ya ‘Ufalme wa Mwenyezi Mungu’, yalifungua njia ya mwanadamu kurejea kwa Mola wake na yakawasilisha simulizi halisi ya Hayat Tayyiba:

Uchumi wa haki: Uchumi unapaswa kuhudumia binadamu, si binadamu kuhudumia uchumi. Kuzalisha mali na ukuaji ni jambo la thamani, lakini matumizi kupita kiasi, anasa na majivuno ni kinyume cha maadili.

Heshima ya binadamu na uhuru wa kweli: Uhuru wa kweli ni kuwa mja wa Mwenyezi Mungu na kuhudumia ubinadamu. Raha ya kweli hupatikana katika ukaribu wa kiroho na Mwenyezi Mungu.

Kupinga kiburi na kudumisha heshima ya Kiislamu: Nguvu ni chombo cha kutekeleza haki na kutetea wanyonge, si kwa ajili ya kutawala na kudhulumu.

Mgongano wa Ustaarabu Katika Kipindi cha Migogoro

Leo hii, ufanisi wa simulizi hizi mbili za ustaarabu katika kukabiliana na migogoro ya dunia unaonekana wazi:

Migogoro ya maadili: Magharibi imezama katika uhalali wa maadili ya mabadiliko; Mapinduzi ya Kiislamu yanasisitiza maadili ya milele na utu wa binadamu.

Migogoro ya utawala: Demokrasia ya Magharibi imekumbwa na siasa za umaarufu bandia, mzunguko wa pesa na madaraka, na uhandisi wa maoni ya umma kupitia vyombo vya habari. Kinyume chake, demokrasia ya kidini huunganisha uhalali wa kimungu na ridhaa ya wananchi, ikisisitiza kuchagua walio bora, ustadi, na ufanisi wa mfumo wa utawala.

Migogoro ya haki: Ubepari wa Magharibi ni mashine kubwa zaidi ya kuzalisha ukosefu wa usawa katika historia. Mapinduzi ya Kiislamu yameweka haki na kupambana na ufisadi katikati ya utawala; hata hivyo, madhara ya mifumo ya Kimagharibi nchini bado yanahitaji marekebisho makubwa.

Migogoro ya kiroho: Magharibi huwasilisha hali ya kiroho bandia na isiyo ya kweli; Mapinduzi ya Kiislamu huwasilishahali ya  kiroho ya Tauhidi, heshima ya binadamu, uja kwa Mwenyezi Mungu, na jihad ya ustaarabu.

Hitimisho: Vita vya Simulizi na Ulazima wa Kurejea kwa Mungu

Mgongano wa leo si wa kisiasa au kijeshi tu; ni “vita vya simulizi za ustaarabu.” Tajriba ya Magharibi imeonyesha kuwa binadamu hawezi kujenga jamii ya haki, usalama na maana bila Mungu. Kinyume chake, simulizi ya Mapinduzi ya Kiislamu huwasilisha kurejea kwa Mungu na utawala wa Tuhidi kama hitaji la kihistoria na kiustaarabu.

Njia ya wokovu kwa binadamu katika zama hizi imo katika muunganiko wa elimu, imani, akili, kiroho, haki na maendeleo. Kuvuka mipaka ya kisasa ya kisekula na kuelekea “mpangilio mpya wa Tauhidi” ndiyo njia ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yameiweka mbele ya binadamu kama mfano hai na wenye uhai – mpangilio ambao imani, elimu, ufanisi, maadili, haki, uwajibikaji na kiroho vinatembea kwa pamoja kwa mshikamano na maelewano.

3494475

captcha